22/07/2021
Wapenzi wafariki wakiwa wamelala chumbani Njombe
MwananchiJul 21, 2021Soma halisi
Njombe. Watu wawili wamefariki dunia mkoani Njombe baada ya kuingia na jiko la mkaa katika chumba cha kulala kwa ajili ya kupunguza baridi.
Hayo yalibainishwa leo Jumatano Julai 21, 2021 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamisi Issah wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya jeshi hilo mkoani hapa.
Alisema marehemu hao waliokutwa na umauti walifahamika kwa majina ya Benitho Mbatha (23) mpiga debe wa mjini Njombe na Jazila Said ambaye kabila ni Mndendeule (27) mkazi wa Namtumbo mkoani Ruvuma.
“Baada ya kufariki hakuna mtu ambaye aligundua k**a kuna watu wamefariki, tukio hili limetokea tarehe 17 mwezi wa saba majira ya saa tano na nusu huko mtaa nwa National Housing kata ya Njombe mjini wakiwa wamelala kwenye chumba kimoja,”alisema Issah.
Alisema sababu ya kifo chao inaonyesha wakati wakiwa hai waliweka moto wa mkaa kwa ajili ya kujihifadhi na baridi ambapo mtindo huo umekuwa ukitumika na watu wengi mkoani Njombe.
Aidha Kamanda Issa alitoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Njombe kutumia njia nyingine kujikinga na baridi na si kuota moto k**a ambavyo wengi wamekuwa wakifanya kwa kwani kufanya hivyo ni hatari kwa maisha yao.
“Niwaombe wananchi wewe unaona chumba chako ni kidogo na unatumia mkaa ndani hiyo ni hatari nyingine na huko lilikotokea tukio chumba ni kidogo na kina dirisha moja na dogo sana. Acheni kulala na jiko ndani ya nyumba sasa hivi ni hatari tafuteni nguo nzito nzito za kuzuia baridi lakini sio moto wa mkaa,”alisema Issah.
Alisema tukio hilo ni la tatu kutokea mkoani Njombe kutokana na tukio jingine kumkuta dada mkazi wa Songea aliyekuwa mhudumu wa baa moja mjini Njombe kufariki ndani kwa jiko la mkaa huku mwingine akifariki wilayani Wanging’ombe kwa jiko la mkaa.
Mmiliki wa nyumba aliyokuwa akiishiri marehemu Benitho Mbata, Amani Samsoni alisema yeye alikuwa wa kwanza kushuhudia tukio hilo baada ya kwenda kumtembelea marehemu na kuwa