21/05/2022
TANZANIA VIONGOZI MNALALAMIKA NA NYIE NDO MNAUWEZO WA KUKATAZA
MLIKATAZA VIROBA LAKINI SAIV KUNA ZA XHUPA YA PLASTIC BAADA YA MIAKA 20 BAADAE TUTAKUWA KWENYE HALI MBAYA KWENYE NGUVU KAZI
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TMDA) imewaonya Watumiaji wa sigara, ugoro na tumbaku dhidi ya athari za kiafya wanazoweza kuzipata ambapo imesema Watu Milioni 8 hufariki kwa mwaka kutokana na Kansa zinazosababishwa na uvutaji sigara huku Watu Mil 1.2 wanaokaa jirani na wavuta sigara wakipata madhara bila ya wao kujijua.
Akizungumza Mkoani Mtwara, Meneja wa TMDA Kanda ya Kusini Dr. Engelbert Mbekenga amesema kwa mujibu wa tafiti za Shirika la Afya Duniani (WHO) takribani Watu Milioni 8 Duniani wanakufa kutokana na Kansa zinazosababishwa na uvutaji wa sigara na 80% ya vifo hivyo vinapatikana katika Nchi zenye uchumi wa chini Tanzania ikiwemo"
"Watu Mil 1.2 wamepata madhara bila wenyewe kujua kwasababu ya kukaa jirani na wavuta sigara na wakati wenyewe hawavuti, kuna umuhimu wa kutoa taarifa kwa wale wanaotaka kuvuta wavute eneo lililojitenga na wengine ili wasiotumia wasipate madhara"
"Kuna madhara makubwa yanayotokana na uvutaji wa sigara ikiwemo Kansa inayoshamnulia eneo la upumuaji, kubadilika kwa meno kuwa machafu wakati wote na msongo wa mawazo"