Mwaki

Mwaki Page maalumu kwa ajili ya hadithi na simulizi mbalimbali za kusisimua

Permanently closed.
HADITHI: CHOZI LA MNYONGEMTUNZI: Mwaki Ze Done.MWANDISHI:Mwaki Ze Done.    Sehemu ya 2.Baada ya askari kuniambia makosa ...
07/07/2021

HADITHI: CHOZI LA MNYONGE

MTUNZI: Mwaki Ze Done.

MWANDISHI:Mwaki Ze Done.

Sehemu ya 2.

Baada ya askari kuniambia makosa yote yanayonikabili nilish*tuka na kudondoka chini baada ya hapo sikuelewa kilichoendelea.
Nilikuja kuzinduka nikiwa nipo hospitalini na pingu mkononi na nilianza kukumbuka nini kilitokea, ndipo nikakumbuka yale maongezi ya mara ya mwisho na afande ambayo yalikuwa hivi

"Ndiyo ni 3 siyo 4"
"Ni yapi hayo??"
"La kwanza unatuhumiwa kwa mauaji, lapili ni ubakaji na latatu ni wizi kwa kutumia siraha za moto"
"Mungu wangu!!! Mimi nimeua??"Nilish*tuka kwa kutajiwa yale makosa nikiwa siamini.
"Ndiyo umeua na ushahidi upo"
"Afande mimi katika maisha yangu sijawahi kuua wala kuiba cha mtu japo Mimi na wazazi wangu ni maskini"
"Ndo k**a ulivyo sikia k**a nawe una ushahidi wa kukanusha makosa yako tueleze??"
"Kwanza afande bado sielewi, nimemuua nani?? Na nimemubaka nani?? Na nimeiba wapi hapo ndio ntajua ushahidi wa kujitetea natoa vipi" nilimwambia yule afande machozi yakiwa yananitoka
"Kwanza umemubaka mtoto wa mama mwenye nyumba, pili uliwatishia wapangaji wenzako na siraha na kuwachukulia vitu vyao, kosa kubwa kabisa ambalo ndo nakusikitia umewaua wazazi wako wote wawili kwa kuwakatakata na mapanga na ushahidi upo"
"Niniiiiii baba na mama wameuawa??" Niliuliza kwa jasiba kwa muda huo nilikuwa nimemukunja yule afande shati lake
"Ndiyo wameuawa na muuaji mkuu ni wewe" Baada ya kuambiwa ivo nilianza kuhisi kizunguzungu na kudondoka.

"Eheee vipi we gaidi umeamuka nilijua Mungu atakuchukua moja kwa moja??" Nilish*tushwa na Doctor nikiwa bado nakumbuka na kutafakari zile tuhuma nilizo ambiwa na afande katika chumba cha mahojiano.
"Doctor mimi siyo gaidi"
"Bana me siyo hakimu wa kunieleza mi ninachojua na nilichoambiwa ni kwamba niwe makini na wewe kwasababu ni mtu hatari na hapo nje kuna askari wa nne kwa ajili ya ulinzi tuu"

Nilishangaa maneno ya Doctor kila kitu niliona ni k**a ndoto ila ndio ulikuwa uhalisia wenyewe, baada ya Doctor kuondoka nilikumbuka habari za wazazi wangu kufa nilianza kupiga kelele mule wodini mpaka maaskari waliokuwa nje waliingia ndani
"Eheee unataka kufanya tena matukio eeeeee??" Aliongea askari mmoja baada ya kuingia ndani

"Afande me sina makosa niacheni nikawaangalie wazazi wangu kijijini kwetu k**a kweli wamekufa" niliongea huku nikiwa nalia k**a mtu aliyechizika

"We umechanganyikiwa eee?? Kwani Doctor hajakwambi??"

Nilitahamaki na swali la askari nilitulinza munkari kidogo na kuuliza
"Hajanambia!!!? Kuhusu nini??"
"Doctor hajakwambi kwamba wazazi wako tayari wameshazikwa??"
"Wamezikwa!!!?? Lini?? " Niliuliza huku nikiwa sielewi askari kitu anachoongea
"Ndiyo wamezikwa, unajua mara baada ya wewe kuzimia kule kituoni ni muda gani umepita mpaka wewe kuja kuzinduka hii leo??"
Nilikaaa kimya huku nikiwa sielewi kila kitu ambacho askari anaongea yaani kila kitu niliona ni k**a tunataniana tuu.
"Unaka kimya eeee?? Ila ndo ujue hivyo hapa hospitali umekaa wiki moja na toka wiki iliyopita ndo umezinduka leo na wazazi wako walizikwa na serikali baada ya ndugu kukosekana"aliongea yule askari na kutoka nje na kuniacha nikiwa nipo kimya ndani. Nilijikuta machozi yanaanza kunitoka tena na nilikumbuka jinsi maisha ya wazazi wangu yalivyo kuwa kijijini na jinsi walivyoniasa kutokuja mjini niliona huuu ndo mwisho wa dunia ambao huwa unazungumziwa. Siku hiyo ilikuwa ni kulia tuu mpaka saa tatu usiku nilikuwa nalia na nilikuwa sijaona mtu yeyote akiingia chumbani kwangu nilipolazwa hata wa kuniletea chakula hakuwepo. Ilifika asubuhi nikiwa sijala kitu chochote na mwili ulikuwa hauna nguvu kabisa, Mara aliingia nesi mmoja akiwa anakuja kwa kunyata huku kabeba chupa ya uji.
"Chukua huu uji kunywa haraka haraka maana tumeambiwa usipewe chakula chochote mpaka kesho ambapo ndo siku ya kwenda mahak**ani" aliongea yule nesi huku akiwa makini asije akash*tukiwa.
Kwakuwa nilikuwa na njaa sana sikutaka kuuliza chochote mpaka nishibe, nilichukua ile chupa nilianza kunywa uji bila hata kumiminia kwenye kikombe wala kujali ni wa moto, yule nesi aliniangalia kwa huruma na kuniuliza
"Hivi ni kweli kaka wewe ndio umefanya yote hayo??"
"Dada mi sijui chochote yawezekana ni kweli au so kweli"
"Mi nikikwangalia kabisa usoni naona siyo wewe, ila kinachoniuma unaenda kufia gerezani"
"Dada k**a ni ivo itakuwa bora zaidi "
"Haya bana mi naondoka ila usimwambie mtu k**a kuna mtu aliingia humu ndani" Yule nesi aliniambia na kutoka nje, ile tuu ndo anataka kufungua mlango alikutana uso kwa macho na mkuu wa kituo cha polisi akiwa na Doctor mkuu wa hospitali, nilimuona yule nesi anatetemeka mpaka chupa aliyokuwa ameificha ili mudondoka.

Je nini kitatokea kwa pendo??
Je itakuwaje kwa kijana jeriko??

Itaendelea.....
Usikose sehemu ya 3

Ili kuisoma hadithi hii chapu kwa haraka tembelea page ya *Mwaki Ze Done Story* au jiunge na group la facebook *hadithi za Mwaki Ze Done*

Contact: 0742138331

HADITHI: CHOZI LA MNYONGEMTUNZI: Mwaki Ze Done.MWANDISHI:Mwaki Ze Done.    Sehemu ya 1.Kwenye maisha kuna changamoto amb...
07/07/2021

HADITHI: CHOZI LA MNYONGE

MTUNZI: Mwaki Ze Done.

MWANDISHI:Mwaki Ze Done.

Sehemu ya 1.

Kwenye maisha kuna changamoto ambazo binadamu hupaswa kuzipitia ili kujua baya na jema, rafiki na adui. Hii ni hadithi ambayo ukiisoma mpaka mwisho utajifunza mengi na utagundua kwamba si kila unachokijua kipo k**a unavyokijua, si kila unachokiona kipo k**a unavyokiona, na Mungu hapangiwi na hutoa kwa muda aupendao yeye.

Mwanzo.

Ilikuwa jumapili asubuhi na mapema nikiwa najiandaa kwenda kanisani, nikiwa nimekaa mlangoni huku nang'arisha viatu vyangu niliwaona maaskari watatu wakiwa wameongozana na Mama mwenye nyumba wakiwa wanakuja upande nilipokuwa nimekaa, sikush*tuka hata kidogo kwani nilikuwa sina kosa hata moja nililolifanya.

"Jamani huyu ndo jeriko, mpangaji wangu k**a nilivyowaambia kazi kwenu" aliongea Mama mwenye nyumba baada ya kufika nilipo kuwa nimekaa akiwaambia maaskari aliokuwa ameambatana nao.
"Jeriko upo chini ya ulinzi" aliongea askari mmoja huku akiwa anaonesha kitambulisho chake.
"Heeeee!! Chini ya ulinzi tena kwa kosa lipi??" Niliuliza huku nikiwa sielewi kinachoendelea.
"Inuka kwa amani tuondoke kosa utalijua kituoni" askari aliongea kwa ukali huku akiwa ananisogelea. Kwa kuwa nilikuwa mtu muoga sana linapokuja swala la maaskari niliamua kutii sheria bila shuluti, niliamua kuweka viatu vyangu ndani na kufunga mlango tukaanza safari ya kuelekea kituoni. Baada ya k**a nusu saa tulikuwa tupo kituoni na shauku yangu kubwa ilikuwa ni kutaka kujua kosa langu kubwa ni lipi mpaka naletwa sehemu hii.

"Bwana jeriko wewe ni mtu hatari sana kwenye jamii" aliongea askari.
"Sijakuelewa mkuu hatari kivip??"
"Usiwe na Papara utaelewa tuu muda ukifika" aliongea askari huku akiniamulu nivue viatu na mkanda kwa ukali, nilivua huku nikiwa na hofu kubwa na sielewi kosa langu ni lipi
"Samahani afande kosa langu ni lipi??" Niliuliza.
Badala ya kujibiwa nilianza kuchezea kichapo cha maana kutoka kwa askari, nilipigwa sana mpaka mwili ukalegea na mwishowe nikatupwa sero bila hata kujua kosa langu.
Zilipita dakika, masaa hatimaye siku ikakata, juma tatu asubuhi mida ya saa nne ndo nikazinduka toka usingizini maana nilichelewa kulala kutokana na maumivu niliyokuwa nayo.

"Jamani mnavyofanya mjue siyo vizuri kabisa"
"Alafu wewe hatutaki mambo ya kitoto sisi, ko unatupangia kazi??"
"So ivo mnakiuka Sheria iweje mpige hivi kijana wa watu kwa tuhuma zisizo eleweka na mumemtupa sero bila hata kumwambia makosa yake"
"Eheee ko we lako unasemaje??"
"Afande kasimu achana na mpuuzi huyo sisi tunafanya kile tulichoagizwa na mkubwa"
Yalikuwa ni mabishano ya maafande ambayo niliyasikia punde tu baada ya kuzinduka toka usingizini.
Zilipita k**a dakika kumi nilikuja kuchukuliwa na kupelekwa kwenye chumba cha mahojiano

"Jeriko unajua makosa yako??" Niliulizwa na askari ambaye alionekana ni wa tofauti na wale waliokuja kunik**ata jana

"Sijui afande"
"Duuuu!! Pole sana nakuonea hadi huruma"
"Tafadhali afande naomba niweke wazi tuu angalau hata nijue"
"Kwanza bwana jeriko wewe una makosa 3 k**a so 4"
"Heeeeeee!!!! Makosa 4!!!!?" Nilish*tuka huku nikiwa nimemutolea hicho yule afande
"Ndiyo ni 3 siyo 4"
"Ni yapi hayo"

Baada ya askari kuniambia makosa yote yanayonikabili nilish*tuka na kudondoka chini baada ya hapo sikuelewa kilichoendelea.

Je ni makosa gani jeriko alitajiwa??
Na nini kilitokea baada ya jeriko kudondoka??

Usikose sehemu ya 2

Ili kuisoma hadithi hii chapu kwa haraka tembelea page ya *Mwaki Ze Done Story* au jiunge na group la facebook *hadithi za Mwaki Ze Done*

Contact: 0742138331

05/07/2021

Special pages kwa ajili ya hadithi kali na za kusisimua

Address

Songwe

Telephone

+255742138331

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mwaki posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Mwaki:

Share


You may also like