ELIMU YA NDOA Naomi Andrew

ELIMU YA NDOA  Naomi Andrew KARIBU TUYAJENGE NA SIO KUYABOMOA

    Mwanaume anapaswa kujua kwamba hakuumbwa ili kumkandamiza mke bali kumpenda (kuwa tayari kufa kwa ajili yake) na kum...
16/10/2022





Mwanaume anapaswa kujua kwamba hakuumbwa ili kumkandamiza mke bali kumpenda (kuwa tayari kufa kwa ajili yake) na kumtambua k**a sehemu ya mwili wake.

Hiki ni kipindi cha hatari sana, wanawake wengi wanapigania haki sawa. Harakati za wanawake zimeenea k**a moto wa nyika, wakidai kwamba mbali na suala la wanawake kuzaa, hakuna tofauti yao na wanaume. Ni chungu cha moto katika ndoa ambazo mwanamke na mwanaume wote wanataka kuwa viongozi. Kuna methali inasema mafahari wawili hawawezi kuishi z**i moja. Hii ndio sababu ndoa nyingi za leo zinapita katika moto. Wanaume wengi wanakabiliwa na changamoto ya kuwa na wanawake wanaowazidi vyeo au kipato, au vyote kwa pamoja. Na kwa kweli kadiri wanawake wengi wanavyozidi kuongeza viwango vya elimu, kuongezeka kiuchumi na kupanda vyeo ndivyo wanavyoongeza shauku ya kuwatawala waume zao. Ni ukweli usiopingika, mwanaume anahitaji ujasiri na ufahamu wa ziada ili kuishi bila matatizo yoyote na mwanamke wa jinsi hiyo.

Mapambano ya fursa sawa kwa wanaume na wanawake yameenea kila kona ya dunia. Inawezekana jambo hili likawa jema kwa wanawake ambao wasingependa kukandamizwa au hata kuongozwa pasipo kukandamizwa. Na kwa upande wa pili, pengine jambo hili linaweza kuhesabiwa k**a laana au mzigo kwa wanaume ambao wasingependa kuona wanawake wakifanikiwa zaidi yao na kufurahia uhuru wa ‘kuwa mwanadamu’ k**a alivo mwanaume. Vyovyote itakavyokuwa, matokeo hasi au chanya yatatokana na mtazamo alionao mwanaume juu ya mwanamke. Kwa mfano, wanaume wengi huanza kujihami pale wanapohisi mwanamke anakuwa juu. Hebu tafakari kauli zifuatazo; “Hivi unajua kuwa mimi ndio baba wa familia?” “Au unanidharau kwa sababu una pesa nyingi? / Umesoma?” Mwanaume anapohisi kupoteza nafasi yake k**a kiongozi kwa sababu yoyote ile, huo ndio wakati ambao amani ya nyumba huanza kutoweka. Ataacha kumpenda mke wake, ataacha kumsikiliza, ataathirika kisaikolojia na mwisho utakuwa mbaya kwa familia nzima.

MWANAMKE MWENYE BUSARA (MITHALI 14:1)​
Hata k**a ana cheo hawezi kufanya maamuzi katika familia bila kumshirikisha mume wake (Mithali 14:1)​
Humtii mume (Efeso 5:22)
Hawezi kuwa mropokaji asiyetafakari kabla ya kuzungumza jambo kwa mumewe (Mithali 9:13).​
Ni fahari kwa mke kumstahi mume wake asiabike kwa lolote. (1 Samweli 25:25)​
Ni fahari kwake kuongeza kipato cha familia. (Mithali 31:14)​
Ni faraja kwa mumewe. (Mithali 15:17)​
Ni msikivu, haoneshi dharau na majivuno kwa mumewe (hafanani na Vashti, Esta 1:12​

Mwanaume Unatakiwa Ufanye Nini?

Jenga mtazamo chanya, jiamini na uwe mpenda maarifa (Mtu thabiti). Tambua kwamba mwanamke hakuumbwa kuchukua nafasi yako, hana mpango huo na k**a akitaka hawezi kufanikiwa.
Tambua kuwa mwanamke ameumbwa kwa ajili yako (1 Wakorintho 11:9)
Hakikisha unakuwa msimamizi na mshauri mzuri wa mwanamke katika cheo, mali au pesa zake.
K**a kiongozi wa familia, ongoza majadiliano kuhusu mipango ya maendeleo ya familia, malezi ya watoto na utawala bora wa familia.
Usitegemee kwa asilimia zote kipato cha mke wako, bali iwe ni nyongeza tu kwa familia. Kwa lugha nyingine ni kwamba, unatakiwa uweze kuhakikisha unatoa mahitaji muhimu ya familia bila kumtegemea mke wako.

Jenga uhusiano mzuri wa kimapenzi na kifamilia ili mfikie kiwango cha kutokuwa wabinafsi na kuwa shirika/kitu kimoja katika kila kitu kiingiacho na kutoka katika ndoa yenu. Hili linawezekana pale ambapo upendo wa dhati na hofu ya Mungu inapokuwa nguzo ya mahusiano yenu.
Jenga mawasiliano mazuri na ya wazi kwa kila kitu kati yako na mke wako. Mpe nafasi ya kuelewa kipato chako, akiba yako pamoja na juhudi na mipango uliyonayo kwa ajili ya maisha yenu ya baadaye. Weka wazi hisia zakounapohisi anaididimiza chini nafasi yako. Ni wanawake wachache sana wanaofurahia kuishi na mwanaume asiye na mipango.

K**a bado hujaoa lakini mchumba wako anakuzidi kipato, ongea naye vizuri, mweleze msimamo wako, mitazamo yako na mkubaliane jinsi mtakavyoishi maisha yenu k**a mume na mke. Mke anapaswa kujiandaa kuongozwa hata k**a ana kipato, cheo au mali nyingi kuliko mume.

Kwa nini MUNGU alimwambia Hosea aoe kahaba (/ MalayaHosea 1:2)?Katika Hosea 1:2  tunasoma, “BWANA akamwambia Hosea, ‘Nen...
07/10/2022

Kwa nini MUNGU alimwambia Hosea aoe kahaba (/ MalayaHosea 1:2)?

Katika Hosea 1:2 tunasoma, “BWANA akamwambia Hosea, ‘Nenda ukajitwalie mke wa uzinzi na uzae watoto wa uzinzi.’” Hosea alitii, akaoa mwanamke aliyeitwa Gomeri, ambaye hakuwa mwaminifu kwake. Kwa nini Mungu alimwambia Hosea aoe kahaba?

Kuanza, ni muhimu kutambua amri hii inaweza kueleweka kwa njia mbili tofauti. Kwanza, na uwezekano zaidi, amri hii inaweza kuwa moja ya kutarajia. Kwa maneno mengine, huenda Mungu alimwagiza Hosea kuoa mwanamke ambaye baadaye angekosa uaminifu kwake. Uwezekano mwingine ni kwamba amri ilikuwa kwa Hosea kuoa mtu ambaye tayari anajulikana kuwa kahaba.

Vyovyote vile, sababu ya agizo hilo lisilo la kawaida yatajwa katika nusu ya mwisho ya mstari uleule: “Kwa maana nchi imefanya uasherati mwingi kwa kumwacha BWANA.” MUNGU alitaka kutoa kielelezo cha uhusiano wake na watu wa Israeli, ambao hawakuwa waaminifu Kwake kwa kuabudu sanamu. Mada hii inafanywa kupitia sehemu iliyobaki ya unabii katika sura ya 1 na mjadala wa ukosefu wa uaminifu wa Israeli katika sura.

Katika Hosea 3:1, baada ya Gomeri kumwacha Hosea na kuishi katika uasherati, Bwana alimwamuru Hosea amtafute na kumnunua tena. MUNGU alikuwa akiendeleza kielelezo chake, isipokuwa sasa alitaka kuonyesha ukuu wa neema yake: “K**a vile BWANA anavyowapenda wana wa Israeli, wajapoigeukia miungu mingine.” Upendo mwaminifu wa Hosea kwa Gomeri ulikuwa kielelezo cha uaminifu wa MUNGU kwa Israeli waasi. K**a vile Gomeri hakuwa mwaminifu kwa mume wake na kulazimika kukombolewa, Waisraeli walihitaji hatua ya MUNGU ya kurejesha uhusiano wao.

Nabii Hosea aliamriwa kuoa mke asiye mwaminifu, na hilo liliweka kielelezo cha uhusiano uliovunjika wa Israeli pamoja na MUNGU. Israeli walikuwa wamechaguliwa na kupendwa na MUNGU lakini hawakuwa waaminifu Kwake kwa njia ya ibada ya sanamu. K**a vile Hosea alivyomkomboa mke wake aliyeachana naye na kutaka kuendeleza uhusiano wake naye, MUNGU aliahidi kuwakomboa Israeli na kufanya upya uhusiano wao pamoja naye. Hadithi ya Hosea na Gomeri ni picha isiyosahaulika ya upendo wa MUNGU wenye nguvu na usio na mwisho kwa watu Wake wa agano.

WANANDOA HAKUNA UPENDO BILA HESHIMA1. Joshua 24: 1-2. 15-18 Waefeso 5: 21-32 Yohane 6: 60 – 69 Mahubiri Yamejikita katik...
14/09/2022

WANANDOA HAKUNA UPENDO BILA HESHIMA

1. Joshua 24: 1-2. 15-18 Waefeso 5: 21-32 Yohane 6: 60 – 69

Mahubiri Yamejikita katika Haya Zifuatazo
“Kila mmoja amstahi mwenzake kwa sababu ya heshima mliyo nayo kwa Kristo” (Waefeso 5: 21).
“Mke anapaswa kumheshimu mumewe” (Waefeso 5:30).
“Nanyi waume wapendeni wake zenu k**a Kristo alivyolipenda kanisa, akajitoa mwenyewe sadaka kwa ajili yake” (Waefeso 5: 25).

MWANANDOA UKIHESHIMIWA JIHESHIMU

Mwanamke asiyekuwa na heshima kwa mume wake huyo ni bora mwanamke na sio mwanamke bora. Mwanaume asiyekuwa na heshima kwa mke wake huyo ni bora mwanaume na sio mwanaume bora. Paulo aliwaasa wanaume, “Nanyi wanaume, katika kuishi na wake zenu mnapaswa…mwatendee kwa heshima” (1 Petro 3: 7). Heshima ni kitu cha bure. Heshima haiwezi kuuzwa na wala kununuliwa. Mwanaume anayemheshimu mke wake atamlinda. Mwanaume anayemheshimu mke wake hatamwaibisha mbele ya watu. Vilevile mwanamke anayemheshimu mume wake hatamwaibisha mbele ya watu.

Niliwahi kumwona mwanaume mmoja anamfungulia mlango wa gari mke wake. Nililiona hilo kuwa tendo la heshima na nilipomsifia mwanaume huyo mbele ya mke wake kwa kumpa heshima hiyo mke wake. Mke wake aliniambia kuwa hapo hamna heshima ila mlango wa gari umeharibika unafunguliwa kwa nje. Usingoje vitu viharibike ndipo ufanye mambo ambayo yanaashiria heshima.

Heshima kitu cha bure. Ni methali ya Kiswahili inayomaanisha kuwa heshima haiwezi kununuliwa wala kuuzwa. Mtu hufanya heshima kwa mapenzi yake. Kila ndoa ina shetani wake na malaika wake. Ukosefu wa heshima ni shetani wa ndoa na heshima ni malaika wa ndoa.

Mwanaume kumuita mke wake k**a glasi au chupa sio heshima. Mfano kumuita Anna au Terezia badala ya Bibi Terezia, Bibi Anna au Mama John. Na vivyo hivyo mwanamke kumuita mume wake k**a sahani sio heshima. Mfano kumuita Benard au Denis badala ya Bwana Bernard au Bwana Denis au Baba Agnes. Sara mke wa Abrahamu katika Biblia alimuita mume wake kwa heshima. “Sara kwa mfano alimtii Abrahamu na kumuita Bwana” (1 Petro 3: 6). Utii na heshima sio deni la kulipwa na mwanamke tu bali ni deni la kulipwa na mwanaume pia. Heshima lazima itolewe na pande zote mbili.Mwanaume kumtaharifu mke wake juu ya safari zake ni heshima. Asipofanya hivyo ni dharau kwa yule ambaye hana budi kumheshimu. Angalisho hapa ni kuwa katika baadhi ya tamaduni k**a tamaduni za watu wa Amerika kumuita mtu kwa kutumia jina lake la kwanza ni heshima.

Heshima ni wajibu. “Mke anapaswa kumheshimu mumewe” (Efeso 5:30). Niliongea na baadhi ya wanaume wakanielezea jinsi wanavyohisi mwanamke anakosa heshima kwa mume wake akitenda mambo haya: Kwenda nje ya ndoa ni ukosefu wa heshima kwa mume wake. Mwanamke anapopigana na wazazi wa mume wake au kuwatukana matusi hata ya nguoni ni ukosefu wa heshima. Pengine mwanaume akitoka kazini amechoka na mwanamke hajishughulishi na yeye hasemi, “pole na kazi” au “karibu nyumbani,” anaendelea kupiga soga yaani kuzungumza na wenzake kana kwamba hakuna aliyeingia ndani ni ukosefu wa heshima kwa mume wake.

UPENDO NI MOYO WA NDOA HAUPASWI KUSIMAMA

Hakisimami na kikisimama msiba. Ni kitendawili ambacho jibu lake ni moyo. Moyo ni kiungo cha mwili cha kusukuma damu mwilini kote. Moyo usimamapo kiumbe huwa hakina tena maisha. Upendo ukisimama katika ndoa ndoa inakufa. Moyo wa ndoa ni upendo. Wanandoa hawana budi kuwaka mapendo. Moyo wenye kuwaka mapendo unamweka mtu katika mawazo, katika kumbukumbu. Moyo waweza kumaanisha fikira, mawazo, kumbukumbu. Asiyekuwapo machoni na moyoni hayumo. Lisilokuwepo machoni, na moyoni halipo. Ni k**a msemo huu. Amenitoka moyoni. Simpendi tena. Simfikirii tena. Mwanandoa hana budi kumfikria mwenzake na kumweka katika kumbukumbu.

Kuna misemo ya Kiswahili isemayo: Nyumba yenye upendo haikosi bahati. Pendo huleta baraka nyumbani. Moyo wa upendo unawaka mapendo. Biblia yasema: “Nanyi waume wapendeni wake zenu k**a Kristo alivyolipenda kanisa, akajitoa mwenyewe sadaka kwa ajili yake” (Waefeso 5: 25). Katika ndoa lazima uwe tayari kumfia mwenzako. Kuna mwanaume aliyemuuliza mke wake, “Wangu wa moyo unanipenda.” Mwanamke akajibu, “Ninakupenda Sweetie!” Mwanaume akaendelea kuuliza, “Je unaweza kufa kwa ajili yangu.” Mwanamke akasema, “Siwezi, upendo wangu kwako ni upendo usio kufa.”

“Waume wanapaswa kuwapenda wake zao k**a miili yao wenyewe. Hakuna mtu yeyote auchukiaye mwili wake; badala ya kuuchukia, huulisha na kuuvika.” (Waefeso 5: 28 – 29). Mpambe mwenzako apambike. Mwanaume k**a unapenda kuongolea wanawake waliojipamba mpambe mke wako. Kuna methali ya Wahaya wa Bukoba isemayo, “Iwe agonza abarengize tolengya wawe.” “Wewe unayependa wanawake waliojipamba kwa nini haumpambi wa kwako.”

WANANDOA UPENDO NA CHUKI NI K**A MAJI NA MAFUTA
Chuki inajenga kuta. Upendo unajenga daraja. Kuna mwanaume aliyemwambia Padre, “Nataka kumfukuza mke wangu Padre aliuliza, “Amezaa nje ya ndoa.” Baba huyo akasema, “Hapana.” Padre akauliza tena, “Amekuibia?” Baba huyo akasema, “Hapana.” Padre akauliza tena, “Hakuheshimu?” Baba huyo akasema, “Hapana.” Padre akauliza tena, “Nipe sababu kwa nini unataka kumfukuza?” Baba huyo akasema, “Mke wangu simpendi tena?” Padre akauliza kwa mshangao, “K**a ni hivyo kuna siku utasema, watoto wangu siwapendi tena hivyo nawafukaza.” Baba huyo akasema, “Siwezi kamwe hata siku moja kukataa kuwapenda watoto.” Mwanaume huyu alikuwa na chuki. Chuki inajenga ukuta. Kadiri ya Kamusi ya maana na matumizi chuki ni fitina, uchongezi na uchukivu. Mifano: yeye hana chuki na mtu, mjini hapa anapatana na kila mtu. Kwa kutia chuki kazini amewagombanisha wafanyakazi wengi. Biblia ina mengi ya kutueleza juu ya chuki. “Afadhali mlo wa jioni wa mchicha na upendo, kuliko karamu ya nyama nono pamoja na chuki” (Methali 15: 17). “Mwenye chuki huficha chuki yake kwa maneno mazuri, lakini huwa ana hila moyoni mwake. Akiongea vizuri usimwamini, moyoni mwake mna chuki chungu nzima. Huenda akaficha chuki yake, lakini nia zake mbaya zitajulikana kwa wote” (Methali 26:24-26). “Chuki huzusha ugomvi lakini upendo hufunika makosa yote” (Methali 10:12).

Wazazi nimejifunza sisi  adui namba moja wa kumharibu mtoto au watoto, kwa nini nasema hivyo? Hii ni kwa sababu Wazazi t...
08/09/2022

Wazazi nimejifunza sisi adui namba moja wa kumharibu mtoto au watoto, kwa nini nasema hivyo? Hii ni kwa sababu Wazazi tunakila sababu ya kuwajibika katika malezi ya mtoto au watoto. Wapo Wazazi ambao wanadiriki kusema kuwa huyu mtoto amenishinda, mbele ya huyo mtoto unafikiri hapo unamtengenezea mtoto mazingira gani na wewe pia unajitengenezea mazingira gani?



Mambo muhimu ya kuzingatia katika malezi;

1 . ) Mpe malezi bora
Mlee katika njia impasayo naye hatoiacha mpaka atakapokuwa mzee. Mlee kwa upendo naye atakulipa kwa upendo, hakika mtoto wako ukimlea vizuri anafuata maadili mazuri na maadili mazuri anayapata kutoka kwa mzazi, waweke watoto wako katika hali ya usafi hata mgeni akitokea atavutiwa na mtoto wako na hata kumpakata kuliko kumuacha mtoto mchafu muda wote hana uangalizi anacheza katika mazingira hatarishi. Wazazi siyo vema kuwatukana watoto chunga sana ulimi wako, unapomtukana mtoto anaiga matusi na tabia mbaya kutoka kwako mzazi, ataona ni kitu cha kawaida hata mama au baba anafanya. Kwa mfano wazazi wengine wanawatukana watoto wao k**a vile, ashakumu si matusi (naomba uniwie radhi kwa maneno haya) mbwa wee, mshenzi wee na matusi mengine ambayo matusi hayo yanawaharibu watoto kiakili kabisa hatimaye watoto wanaathirika kisaikolojia.

2) Mfundishe mtoto jinsi ya kuvua samaki na siyo kumpa samaki
Anza kumjengea tabia nzuri mtoto angali akiwa mdogo mpe njia za kufanikiwa, wewe k**a mzazi umepitia mengi hivyo basi kupitia makosa yako umejifunza mengi sana kwa hiyo mfundishe mtoto apite njia nzuri ili asije kurudia makosa k**a yako ,mfundishe mabadiliko ya yanayoendelea duniani ili ajiandae na mabadiliko hayo. Usimlee tena katika mfumo wetu wa elimu ambapo unaandaliwa kuwa mwajiriwa, mlee katika mawazo ya kujitegemea, kujiajiri, jinsi ya kuona fursa katika jamii na kuzitendea kazi, jinsi ya kutengeneza ajira na siyo kuajiriwa tu kwani kazi za maofisini siku hizi zimekuwa changamoto hivyo basi ni vema kumwandaa mwanao katika mabadiliko haya ambayo yapo na yataendelea kuwepo.

3 . ) Mfundishe mtoto kukosa
Maisha ya binadamu ni mafupi kwa hiyo huwezi kukaa na mwanao siku zote inakupasa kumfundisha mtoto kukosa pia wakati mwingine ni vizuri sana mfano mtoto anataka kitu fulani analia ameshasoma saikolojia yako mzazi, wewe ukiona tu mtoto analia unamtimizia hata k**a kitu siyo cha maana anampa tu hata k**a una hela muda mwingine mwambie sina ili ajifunze kukosa mpe hata siku nyingine ,Waingereza wanasema hivi’’ teach your child to learn or to face disappointment’’ maana yake tuwafundishe watoto kukosa au kukutana na changamoto ili wajifunze.

4. ) 5. Mwisho, wape watoto chakula bora ambavyo vitawapa afya bora ya mwili na kinga dhidi ya magonjwa na hapa nazungumzia vyakula vya asili na siyo vya viwandani k**a vile matunda, mboga za majani na siyo soda, p**i biskuti nk. Mpe mtoto ratiba ya kusoma vitabu au mambo yake ya darasani .

  Jinsi Ya Kuwa Baba MzuriNi jambo la kawaida kwa wazazi wa mara ya kwanza kushangaa jinsi ya kuwa baba mzuri kwa watoto...
04/09/2022



Jinsi Ya Kuwa Baba Mzuri

Ni jambo la kawaida kwa wazazi wa mara ya kwanza kushangaa jinsi ya kuwa baba mzuri kwa watoto wao na kuwa Mume mzuri kwa Mke aliye jifungua. Pia wangependa kufahamu jinsi ya kuwa na familia zenye mshik**ano na furaha. Makala haya yana kudokezea jinsi ya kutimiza haya yote!

1. Hakikisha kuwa unatenga wakati wa kuwa na familia yako

Kazi ni muhimu na ni vizuri kufanya kazi kwani hiyo ndiyo njia pekee ya kuwa hakikishia wana jamii wako maisha mema. Ila, ni vyema kukumbuka kuwa familia yako ni muhimu na mshik**ano kihisia ni muhimu hasa sasa alipojifungua mtoto Mke wako . Kazi huenda ikaisha lakini familia yako itakuwepo nawe wakati wote, hakikisha kuwa unawapatia wakati wako. Katika wakati wenu wa pamoja, mnaweza fanya mambo ya kusisimua yanayo wafurahisha. K**a vile kupika pamoja, kusoma vitabu, kutazama kipindi mnacho kipenda ama hata kutembea.

2 . Ni vyema kuchukua wakati wa mapumziko

Mbali na kuwa mzazi wa mara ya kwanza, wewe bado ni binadamu na sio mashine. Na k**a binadamu wengine, kuna nyakati ambazo utahisi umelemewa na mambo ama una mambo mengi yanayo hitaji umakini wako. Kazi, mke wako, mtoto wako, wakati mwingine marafiki ama ndugu zako, yote haya ni mengi kwa mtu mmoja. Ukihisi kuwa mambo yamekulemea, ni vyema kuchukua muda kuwa peke yako na kupumzika. Kufanya hivi kutakusaidia kupata nishati zaidi na kuanza upya tena. Usione haya kuchukua muda na kupumzika.

3 . Kuwa na wakati wa kucheza na watoto wako

Kila jioni unapo toka kazini, chukua dakika chache ucheze na watoto wako, huku ukiuliza walivyo shinda. Njia hii inakusaidia kuwa na mshik**ano mzuri na watoto wako na pia kupunguza fikira nyingi za siku yako na kazi. Na watoto wako wata kupenda!

4 . Kuwa mvumilivu na uzungumze na Mke wako

Kupata mtoto kutaleta hisia nyingi na huenda mazungumzo yenu yaka didimia katika kipindi hiki kwani majukumu pia yame ongezeka. Kumbuka kuwa kuzungumza na mwenzio kutawaleta pamoja na kukusaidia kujua unako hitajika kumsaidia. Kuwa mpole kwa Mke wako kwani bado anapona baada ya mchakato wa kuchoshwa na kujifungua.

5 . Msaidie Mke wako

Kuna baadhi ya wanaume wanao amini kuwa mtoto ni jukumu la mama. Kumsafisha, kumlisha, kumbeba, kumlaza na kazi zingine zote. Hii ni njia isiyo faa ya kufikiria. Kumbuka kuwa mtoto ni baraka kwa wazazi wote wawili. Msaidie mama kufanya kazi zingine na usiwe na uwoga wa kumshika ama hata kumbeba mwanao.

6 . Zungumza na wababa wengine kuhusu safari yao ya ulezi

Kuna vikundi vingi vya wazazi wa mara ya kwanza, utapata ushauri kutoka kwao na ni vyema kuwa na mtu ambaye unaweza muuliza swali kuhusu ulezi. Kwa hivyo usione haya kujiunga na wazazi wengine.

  Jinsi ya Kufanya Ndoa Yako IMARA Wakati wa mwanzo wa maisha ya ndoa, mara nyingi wanandoa hawawezi kufikiri kuwa wanap...
04/09/2022



Jinsi ya Kufanya Ndoa Yako IMARA

Wakati wa mwanzo wa maisha ya ndoa, mara nyingi wanandoa hawawezi kufikiri kuwa wanapaswa kufanya kazi ili kuendeleza uhusiano wao wa upendo. Lakini baada ya muda, tunaona kwamba kudumisha ndoa yenye afya, imara inahitaji juhudi kali.

Wanandoa , hisia imara ya kujitolea ni kiungo muhimu cha kufanya ndoa kudumu milele. Hatua zifuatazo zitakusaidia kuendelea na miaka, kukua na nguvu wanandoa na katika kutembea kwako kwa imani katika MUNGU

Hatua za Kujenga Ndoa YENU

- Sala pamoja

Kuweka kando wakati kila siku kuomba na Mume/Mke wako.

Mume/Mke gundua kuwa jambo la kwanza asubuhi ni wakati mzuri kwenu nyinyi. Kumwomba MUNGU kuwajaza na ROHO MTAKATIFU na kuwapa nguvu kwa siku ya mbele. Inawaletea karibu pamoja mnapojaliana kila siku. Wadhani juu ya nini siku ya mbele inashikilia mpenzi lenu? Ni MUNGU. Upendo wenu huenda zaidi ya eneo la kimwili kwa ulimwengu wa kihisia na kiroho. Hii inaendeleza urafiki wa kweli na kila mmoja na kwa MUNGU pia.

Labda wakati bora kwanu wanandoa unaweza kuwa tu kabla ya kwenda kulala kila usiku. Haiwezekani kulala na hasira wakati mumeshikana mikono pamoja mbele ya MUNGU.

- Kusoma Pamoja

Tengeni kando wakati kila siku, au angalau mara moja kwa wiki, kusoma Biblia pamoja.

Hii pia inaweza kuelezwa k**a wakati wa ibada . Miaka mitano iliyopita familia moja ilianza kuweka muda kila asubuhi ya asubuhi ya wiki kusoma Neno la MUNGU. Baada ya kulipata somo kwenye Seminar niliyofundisha hapa jijini London Uingereza. Wakisoma Biblia na kuomba pamoja-wakati wa ibada ya wanandoa. Kila mmoja ana soma Neno la MUNGU kutoka kwenye Biblia , na kisha tunatumia dakika chache katika sala pamoja.

Wamekuwa wakijitolea kuinua kutoka usingizi dakika 30 mapema ili kufanya hivyo, walitoa ushuhuda siku moja kwenye Seminar nyingine baada ya miaka 3 wa uendelezo wa kumkaribia MUNGU kwa desturi hiyo umekuwa ni wakati wa ajabu sana kwao walikiri wa kuimarisha ndoa yao . Ilichukua miaka 3 kukiri wazi mbele za MUNGU na wanadamu kuwa hakika KUMTEGEMEA MUNGU NI FAIDA, furaha aliyokupa YESU KRISTO shetani hawezi kuiondoa , amani aliyokupa YESU KRISTO shetani hawezi kuiondoa .

3 - Fanya Maamuzi Pamoja

Jitolea kufanya uamuzi muhimu pamoja.

Sizungumzii juu ya kuamua juu ya nini cha kula chakula cha jioni. Maamuzi makuu, k**a ya kifedha, ni bora kuamua k**a wanandoa. Moja ya maeneo makubwa ya matatizo katika ndoa ni nyanja ya fedha. Wanandoa yapaswa kujadili fedha zenu mara kwa mara, hata k**a mmoja wenu ni bora katika kushughulikia masuala ya vitendo, k**a kulipa bili na kusawazisha matumizi mbalimbali. Kuweka siri juu ya matumizi itawaendesha kwenye matatizo, migogoro na chuki wanandoa kwa kasi zaidi kuliko chochote.

Ikiwa unakubaliana kuja na maamuzi ya pamoja juu ya jinsi fedha zinavyotunzwa, hii itaimarisha uaminifu kati Mume na Mke . Pia, huwezi kuweka siri bali kutoka kwa kila mmoja ikiwa mwajiandaa kufanya maamuzi yote ya familia muhimu pamoja. Hii ni mojawapo ya njia bora za kukuza imani k**a wanandoa.

4 - Kuhudhuria Kanisa Pamoja
Shirikini i katika kanisa pamoja.

Tafuta mahali pa ibada ambapo Mume/ Mke mtaabudu , sio tu kuhudhuria pamoja, lakini kufurahia maeneo ya maslahi ya pamoja, k**a vile kutumikia katika huduma na kufanya kufahamiana na watu mbalimbali katika kusanyiko pamoja . Biblia inasema katika Waebrania 10: 24-25, kwamba mojawapo ya njia bora zaidi tunaweza kuimarisha upendo na kuhimiza matendo mema ni kwa kuwa mwaminifu kwa Mwili wa Kristo kwa kukutana pamoja mara kwa mara k**a waumini.

5 - Endelea kudumisha Ndoa yenu

Pangeni kado muda maalum, mara kwa mara kuendelea kuendelea na upendo wenu.

Mara baada ya ndoa, mara nyingi wanandoa upuuza Upendo kwa kuendekeza mazoea wanatelekeza eneo la upendo, hasa baada ya watoto kuzaliwa. Kuendeleza maisha ya urafiki inaweza kuchukua mpango wa kimkakati kwa sehemu yenu k**a wanandoa, lakini ni muhimu kudumisha ndoa salama na ya karibu.

Kuweka romance yako hai pia kuwa ushuhuda wa ujasiri wa nguvu ya ndoa yako ya Kikristo. Endelea kumkumbatia, kumbusu, na kusema kuwa ninakupenda mara nyingi. Kusikiliza Mume/Mke wako, jifunzeni kutunza jembe zenu za WhatsApp mlizotumiana zenye mahaba kwani hizo ni kiberiti za kuwasha moto wakati pale ubaridi wa ndoa kupoa unapo wajia , ujumbe hizo ni kichocheo madhubuti cha kuipa joto ndoa yenu , na kuwakumbusha nyakati za msisimuko wa Upendo usio poa wala Upendo hauhesabu mabaya , Upendo usitiri wingi wa dhambi , Upendo ufurahia nyakati zote , Upendo uvumilia yote , Upendo haukihesabihi haki , chukueni matembezi ufukwe ya I bahari pamoja . Shikaneni mikono kwa upendo . Endeleeni kufanya mambo ya kimapenzi ya umoja sio yale ya ubinafsi.

Hitimisho
Hatua hizi zinahitaji jitihada za kujitolea kwa sehemu zote Wanandoa. Kuzingatia na Kudumisha muendelezo katika upendo kunaweza kuonekana kuwa vigumu, lakini mkiweka ndoa yenu katika MUNGU ni misingi imara , ROHO WA MUNGU atachukua nafasi na kazi kuiimarishs ndoa yenu . Habari njema ni kujenga ndoa yenye afya na huwezi kujenga nje ya uwezo wa MUNGU

ZINGATIO
Tafuteni nini Biblia inasema kuhusu ndoa mara kwa mara musiache nafsi zenu na njaa , zibisheni nafsi zenu maneno ya MUNGU . Mmoja wenu akisikia njaa ya kufanya lisilofaa Neno la MUNGU ni chakula cha Uzima ushibisha nafsi na kuupa nguvu mwili , MUNGU anasema katika Mwanzo 4:6-7
Mwenyezi-MUNGU akamwambia Kaini, “Kwa nini umekasirika, na kwa nini uso wako umekunjamana? Je, ukitenda vyema hutakubaliwa? Na usipotenda vyema, basi, dhambi inakuvizia mlangoni; inakutamani, lakini unapaswa kuishinda.”

  Familia nzuri na yenye amani hujengwa kutokana na uhusiano thabiti wa wanafamilia hasa baba na mama Watoto hujifunza k...
04/09/2022



Familia nzuri na yenye amani hujengwa kutokana na uhusiano thabiti wa wanafamilia hasa baba na mama

Watoto hujifunza kutokana na matendo ya wazazi wao, k**a watoto wakilelewa kwenye familia yenye mifarakano na kutokuelewana baina ya wazazi wao mara nyingi watarithi tabia hizo. Wakilelewa kwenye familia zenye mahusiano mazuri, majibizano yenye kuheshimiana nao watathamini umuhimu wa mahusiano. Tatizo kubwa linalopelekea mahusiano kuzorota ni mawasiliano dhaifu. Udhaifu wa mawasiliano tunaozungumzia ni pamoja na kukaripiana, kutukanana, kununiana na hata kusonyana mbele za watoto wenu.

Hili laweza kuwa tatizo la mahusiano yenu, lakini kwa nini muwahusishe watoto? Kwani ugomvi lazima ufanyike sebuleni? Hakuna faragha k**a chumbani mkakaa na kuzozana?

Kupaziana sauti mbele ya watoto wako inawaletea watoto madhara mbalimbali ikiwemo nidhamu ya uoga na kutojiamini na hivyo kumyima fursa ya kuwa mdadisi na kudhoofisha uwezo wa akili yake kukua kadiri ya umri wake. Kwa maneno mengine, unamdumaza mwanao kwa wewe kutohsiana vyema na mzazi mwenzio. Wewe ni mama au baba kwa mtu na si vinginevyo. Hivyo majina mnayoitana mkiwa na mihasira yenu yanawaondolea uhalisia na heshima mbele za watoto wenu.

Inawezekana kabisa mzazi mwenzako ni mkorofi na hajali k**a kuna mahitaji ya watoto na familia kwa ujumla. Ingawa tunatambua umuhimu wa kushirikiana katika kulea watoto, busara inahitajika katika kuhusiana na mwenza mkorofi wa namna hii katika ndoa. Haingii akilini kwa baba au mama kumcharaza mboko mwenza wake wa ndoa/mzazi mwenza kisa kakosea. Sasa unamcharaza viboko ili ajifunze ama unabomoa mahusiano yenu na maisha ya watoto wenu bila ya wewe kujua?

Suala lingine linaloathiri maadili ya watoto amabalo ni la kimahusiano katika familia ni ubinafsi uliokithiri kwa baadhi ya wazazi. Kuna wazazi ambao wanaishi kwa sheria ndani ya nyumba kwa kuwazuia wenzi wao ikiwemo watoto kutotumia baadhi ya miliki zilizomo ndani ya nyumba zao. Kwa mfano, k**a baba hayupo TV, Radio, nk. haviwashwi ama akiwepo basi woote mnaangalia anachotaka yeye na hakuna mjadala juu ya hili. Bado yote haya ni kutowaheshimu wezi wao wa maisha. Dharau unazomfanyia mwenzio mbele ya watoto wenu unajenga maisha ya watovu wa nidhamu. Watoto namna hii hawatoweza kuwaheshimu watoto wenzao na hata watu wazima ikiwemo waalimu. Matokeo yake watoto hawa itawawia vigumu kusoma darasani na mara nyingi wataishia mitaani kuhangaikia matumbo kwa kugaagaa kuganga njaa ukubwani.

Ikiwa huna mahusiano mema na mkubwa mwenzio vipi utakuwa na mahusiano wa watoto wenu? Watoto pia wanakumbana na changamoto k**a ilivyo kwa watu wazima na wanahitaji mtu wa kuwasikiliza na kuwapa ushauri wa namna ya kuzitatua changamoto hizo. Kutokana na kukosekana kwa mahusiano na mawasilianao mazuri baina ya wazazi na watoto wao, watoto wanapata wakati mgumu kujenga ukaribu na wazazi. Pindi wanapopata changamoto, hasa katika kipindi cha balehe kwa kuogopa kuwahusisha wengi wao hutumbukia katika matatizo makubwa k**a kutumia madawa ya kulevya na mimba za utotoni. Kuna wazazi ambao kwao ni mwiko kuongea na watoto wao ana kwa ana na badala yake husikiliza mahitaji ya watoto kupitia mzazi mwenza! Matokeo yake mtoto akipatwa na matatizo wazazi hawa mara nyingi huishia kuwalaumu wenza wao ambao eti wameshindwa kulea. Mmeshirikiana kuzaa.
Shirikianeni kulea.

Familia nzuri na yenye amani hujengwa kutokana na uhusiano thabiti wa wanafamilia hasa baba na mama. Familia namna hii inayo mazingira muafaka kwa makuzi ya watoto. Ubora wa mawasiliano, uchaguzi wa maneno ya kusema hasa uwapo na hasira mbele za watoto ni muhimu kwa ukuaji na maendeleo ya watoto. Kutofautiana katika mahusiano kupo. Lakini ugomnvi wa maneno kati yenu ufanyeni faraghani, chumbani, n.k. Inawezekana!

Mahusiano mazuri ya wazazi ni muhimu katika malezi ya watoto

Waefeso 5:25, 28-29“Enyi waume, wapendeni wake zenu, k**a Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; Viv...
30/08/2022

Waefeso 5:25, 28-29
“Enyi waume, wapendeni wake zenu, k**a Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao k**a miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, k**a Kristo naye anavyolitendea Kanisa”

Mume kumpenda mke ni agizo. Agizo hili halibadiliki mke akiwa mkorofi, sio mtii au vyovyote vile. Biblia inamuagiza mume ampende mke k**a KRISTO alivyolipenda kanisa. Huu ni upendo mkubwa sana, japokuwa kanisa lilikengeuka mbali naye bado upendo wa KRISTO haukubadilika. Kumpenda mwanamke k**a mwili wako mwenyewe, kumjali na kumtunza.

Ni rahisi sana kwa mwanamke kuonyesha utii pale anapoonyeshwa upendo. Wanaume wengi huonyesha upendo wakiwa wanachumbia ila wakishaoa tu wanajisahau na kusahau k**a mke anahitaji upendo ili aweze kutimiliza majukumu yake k**a mke vizuri kwa furaha. Upendo unaanzia kumjali hisia zake, kumtunza kimahitaji na kumtia moyo, kumsifia na kumuonyesha unamthamini.

Mwanamke anahitaji kujua unampenda kwa wewe kumweleza hivyo kuwa unampenda na kumtendea matendo ya upendo. Wanawake wengi hukosa hamu ya faragha na waume zao kwasababu huona k**a wanapendwa kwa ajili hiyo tu. Mume siku nzima anamkaripia mkewe, hamsikilizi wala kumjali na usiku anaonyesha kuwa anamhitaji saana, huo sio upendo ambao mke anahitaji toka kwa mume wake.

Mume anapoonyesha kumsikikiza na kujali ushauri wa mkewe na kushauriana naye kabla hajafanya jambo lolote mke anaona anapendwa sana na yeye atazidisha upendo na heshima kwa mumewe. Mpende mkeo ili aweze kukuheshimu kwa furaha na sio kwa kujilazimisha. Kumpenda mke ni kujipenda mwenyewe. Mara moja moja mtoe out bila watoto na umueleze unavyompenda, zawadi sio lazima siku ya sherehe au kitu kikubwa, hata chocolate(unanunua kwa ajili yake na sio watoto), mke atahisi kupendwa sana.

  UKIMUESHIMU MUME HUWEZI KUFANYA MAMBO KWA KUMFICHA WAEFESO 5:22-29, 33“Enyi wake, watiini waume zenu k**a kumtii Bwana...
30/08/2022



UKIMUESHIMU MUME HUWEZI KUFANYA MAMBO KWA KUMFICHA

WAEFESO 5:22-29, 33

“Enyi wake, watiini waume zenu k**a kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, k**a Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili. Lakini k**a vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo. Enyi waume, wapendeni wake zenu, k**a Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote k**a hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa. Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao k**a miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, k**a Kristo naye anavyolitendea Kanisa. Lakini kila mtu ampende mke wake k**a nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe.”

Wengi wetu tumeshaisikia mistari hii sana na yumkini hata kuikariri, lakini je ni wangapi wanaiishi? Mistari hii inaanza kuwaasa wake kuwatii waume zao k**a kanisa linavyomtii kristo. Hili ni agizo kwa wake wote bila kujali mume anakutendea nini, anaelimu kiasi gani, anakipato kiasi gani, ameokoka au hajaokoka. Kumtii mume ni kukubali kuwa chini ya uongozi wake, kumwamini anavyoongoza familia, kumstahi na kumheshimu.

Ukimuheshimu mume huwezi kufanya mambo na kumficha, huwezi kumsemesha vibaya mbele za watu, huwezi kufanya maamuzi bila kumshirikisha, utamhudumia katika hali zote kwa upendo bila kumkebehi.

Waume nao wanapaswa kuwapenda wake zao k**a Kristo anavyolipenda kanisa, huu ni upendo mkuu sana. Kristo amelipenda kanisa bila kujali kanisa limemfanyia nini, upendo wa agape. Hata k**a mkeo amekosea kiasi gani, upendo wako lazima uwe mkubwa kuliko kosa lake na uwe tayari kumrejeza kwa upendo, jambo hili sio dogo linahitaji neema ya MUNGU.

Umpende mkeo k**a mwili wako, ukimtunza na kumlisha. Kumpenda katika hali zote, ukimmpenda mke wako utamtunza, utamlinda, utamtia moyo, utahakikisha Ana furaha wakati wote na utajitoa nafsi yako kwa ajili yake bila kujihurumia.

Huu ndio msingi wa ndoa imara, tukifika hapa ndoa zetu zitakuwa zenye amani na furaha siku zote.

Address

Finsbury Park
London
N4L3G

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when ELIMU YA NDOA Naomi Andrew posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share



You may also like