27/04/2024
Jamaa aitwaye Charo alikuwa jirani ya mjombaangu enzi hizo mjomba akiishi kule Kaloleni, Giriama kaunti ya Kilifi.
Charo alipata kazi ya ndani (House Boy) kwa muhindi flani pale Old Town, Mombasa, mambo hayakuwa mabaya kwa wiki mbili za kwanza. Jamaa alikuwa anapiga kazi safi sana.
Sikukuu ya Diwali si ikafika, boss wa Charo akatembelewa na ndugu, majirani na marafiki zake. Charo akaambiwa apange meza ya chakula, baada ya shughuli ya upishi kufana. Charo "ZE SHEF" k**a alivyopenda kuitwa, akaweka vizuri sahani, visu, vijiko, glass za maji lakini akasahau kuweka UMA yaani FORK kwa wenzetu.
Wageni wote wakawa wamekaa kwenye viti vyao tayari kuchapa msosi. Si unajua mambo ya sikukuu baana....mazagazaga kibbaaao!
Charo akiwa nje anapumzika, huku taratibu akinywa juice yake ya passion baridiiiii, Mombasa joto ati. Mara ghafla akasikia sauti ya boss wake.....
BOSS: Hanee Charo lete nyuma veve.....!!!
(Charo hakuamini alichosikia......)
CHARO: Umesemaje Boss?
BOSS: Ve apana sikia mimi, leta nyuma vageni nataka...!!!!!
WEWE UNGEKUWA CHARO UNGEMJIBU NINI BOSS WAKO UKIWA HUKO NJE KABLA KUINGIA NDANI....!!!!! NA UJUE WAGENI WANANGOJA 'NYUMA' HUKO NDANI. 😂