16/09/2022
Habari za Leo wadau Leo nimetafakari sana na kuona Mchango Mkubwa unaotolewa na Bodaboda aidha nimeona Makosa kadha wanayoyafanya Madereva hao pia waendesha pikipiki k**a ifuatavyo:
1.Kukimbiza sana pikipiki sehemu isiyokua na Ulazima
2.Kuvaa malapa au yebo wakati wa kuendesha Bodaboda jambo ambalo ni hatari kwa miguu yao
3.Kutokuvaa kofia ngumu
4.Kutoheshimi sheria za Barabarani hususan vivuko.
Natoa Rai kwa Jeshi letu la Polisi kupitia kitengo cha Usalama Barabarani Kutoa Elimu kwa bodaboda wote aidha wawe na Vituo maalumu na watambuliwe Aidha Walimu wa wanafunzi ambao wako maeneo ya Barabarani kuwasindikiza wanafunzi na kuhakikisha wanavuka salama,utaratibu unaweza kuwekwa kwenye vikao vya wazazi kuona namna nzuri ya kuwasaidia wanafunzi hususan wa Madarasa ya Awali la kwanza na la pili.Mwisho jamii kwa ujumla tushirikiane sote kuwalinda watoto kwa kukemea wanaoendesha vyombo hivyo kwa kasi.INAWEZEKANA kila mtu akitimiza wajibu wake nimejikuta naandika maana nimeshuhudia ajali mbaya sana ya dereva pkpk hapa Morogoro Mvomero Dakawa baada kwakumgonga vibaya sana na sijui k**a atapona mwanafunzi mdogo wa drs la awali shule sijaijua.