Mivumoni kusini

Mivumoni kusini ujenzi wa barabara ya kutoka uwanja wa mpira mivumoni mpaka kwa kanjibai kupitia vangameli,nganya

24/10/2019

Wanamivumoni tumethubutu naamini tumefanikikiwa twendeni tukatekeleze ilani ya chama chetu

25/01/2019

Tupambane kwa nguvu zetu kuhakikisha njia inapitika mwaka mzima sio kwa msimu tu.viongozi wa mtaa tuangalieni na huku sio mpaka maafa yatokee

23/11/2018

daraja la kamto kadogo k**akaburini kwa makamba na lile la kwa mzee chaki ni tatizo

ujenzi wa barabara ya kutoka uwanja wa mpira mivumoni mpaka kwa kanjibai kupitia vangameli,nganya

23/11/2018

kwa sasa wakazi wa mivumoni kusini tunatumia barabara ya madale njia nne

02/11/2018

Habari wanamivumoni kusini.mivumoni kusini nyakati za masika tunakuwa k**a tupo kisiwani ni wakati wa kujipanga tuone madaraja na mito ya vipindi haituathiri wakati wa mvua.viongozi wetu wa mtaa ni k**a wametsahau vle huku mpaka nyakati za chaguzi ndo waje.kwa sasa tuunganishe nguvu zetu wenyewe na baadae tuombe msaada serikali kuu k**a tutakwama sehemu

04/07/2018

Habari wana mivumoni,
Mivumoni ilikuwa ni sehemu salama ya kuishi na hata uwapo njiani/barabarani kusubiri usafiri ulikuwa salama kabisa.hv usalama huo hakuna tena watu wanakabwa na kuporwa kila kukicha.asb,na jioni,maeneo wakabaji walipo viongozi wa mtaa mnapajua ila sijajua kwann hatua hamchukui ili kudhibiti hilo tatizo.

11/06/2018

Upimaji wa viwanja unakaribia kuanza hili ni jambo jema na bei ni rahisi 200,000/ ambayo utalipa kwa awamu tatu 50,000/mara ya kwanza 50,000/ mara ya pili 100,000/ wakati wa kuchukua hati.lakini pia huenda mtaa wetu wa mivumoni ukagawanywa container watakuwa mtaa na mivumoni utakuwa mtaa pia.tujiandae na kujipanga kwa uchaguzi mwaka kesho

21/04/2018

Ndg wananchi hasa sisi tuishio mivumoni kusini.
Baada ya ile mvua ya siku tatu kumalizika imeacha janga kubwa la uharibifu wa barabara.k**a mnavyoijua barabara yetu k**a ukitokea mivumoni mkunguni tatizo linaanzia mitaa ya kwa mzee ngunga hadi makaburini kwa makamba alimaarufu k**a kwa kambwili.kipande hiki hakipitiki kwa gari wala pkpk na wakati mwingine hata waenda kwa mguu lazima wawe na tahadhali kubwa sivyo watavunjika.
Nashauri wakazi wote tujitokeze kurekebisha sehemu korofi na baadae k**a viongozi wataona umuhimu basi wapeleke suala hili halmashauri ili tusaidike kutatua tatizo hili.
Hv mwenyekiti wa serikali ya mtaa wajumbe hawajakuambia tatizo hili la njia?diwani hujui hili tatizo?au baada ya kupata kura hamuonagi haja ya kutembelea wapiga kura wenu ktk mitaa au kwenye kata?

25/03/2018

Habari wana mivumoni kusini
Wakati sasa wa kufanya maendeleo ya mtaa wetu kwa nguvu zetu.mf barabara kutoka uwanja wa mpira hadi huku kwetu.barabara hii ni mhimu sana kwa wakazi wa huku lakini pia ni mhimu kwa wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi eg tofari.cement.nk sasa inapokuwa kwenye hali mbaya hadi kufikia kutopitika ni hatari sana.
Wagonjwa watashindwa kufika hosp kwa wakati.mama wajawazito nao itakuwa tatizo mno.
Shime tujitokeze wkend moja tufanye marekebisho kwenye zle sehemu korofi mf kwa mpagama bonde la mpunga.na kwa mzee chaki hadi kilimani kwa kasele

07/12/2017

mivumoni kusini ni sehemu tulivu yenye amani na upepo mwanana,issue ni barabara zetu wakati wa masika huwezi pita na gari wala bajaj ni changamoto kubwa kwa wamama wajawazito na wagonjwa,viongozi wa serikali ya mtaa angalieni jambo hilo maana hawa ndio wapiga kura wenu,tuwathamini nyakati zote sio kufika huku mpaka kipindi flani barabara hz zinatengenezeka jamani,kuna diwani,mwenyekiti na hata mbunge mkiunganisha nguvu hzo pasina kujali itikadi za vyama mtatutoa kwenye hili tatizo,,,,

07/11/2017

barabara zetu Mivumoni zimeharibika sana wakati mwingine tunalazimika kulipa nauli tsh 1500 kutoka mivumoni mpaka kibaoni,viongozi wa serikali ya mtaa sina shaka hlo mnaliona na lipo ndani ya uwezo wenu,lakini pia ili twende sawa nakumbuka niliwahi kuandika kwenye page hii kwamba pajaj pkpk maarufu k**a bodaboda,na daladala zilipieushuru pale mivumoni centre na mkunguni tangu nimeshauri mpaka leo k**a ushauri wangu ungechukuliwa na kufanyiwa kazi naamini fedha ambayo ingekuwa imepatikana hadi kufikia leo tungeweza kumudu kutengeneza barabara hz na zikapitika bila shida na nyakati zote
*huo ni ushauri wangu*

05/10/2017

Habarini za asb

18/09/2017

Wakati wa masika maji ya mvua yanaharibu sana barabara na hasa daraja dogo linalotenganisha mivumoni Centre na ile ya kusini maarufu k**a kwa mzee Kasele kwa kuelekea makabulini yanayojulikana k**a kwa kabwili Au mkingie, shime wanamivumoni kusini wanaoishi huko na wale wenye maeneo huko tushirikiane kuchangia ujenzi wa daraja hilo mwenye nondo, kokoto, cement nk mnaombwa kuchangia kwa hali na mali ilikuondosha adha ya kutopitika kwa daraja hlo, maendeleo yanaletwa na wananchi wenye mapenzi mema na nchi yao/mtaa Wao,
Jioni njema

04/09/2017

Mtaa wetu wa mivumoni Kwa sasa unawakazi wengi ila kunachangamoto ya shule na kituo cha afya,ni mhimu sasa kuangalia umuhimu wa kujenga shule na hosp

25/06/2017
25/06/2017

Habari za ASB,Wana mivumoni kusini nawashauri tuungane pamoja kutengeneza barabara za mitaa hasa hii mitaa ya kwa shekhe kambwili

16/02/2017

Habarini wana mivumoni

01/10/2016

K**a ningekuwa na uwezo ningeishauri serikali kuugawa mtaa wa mivumoni ili kuwe na mitaa miwili yaani container na mivumoni ili iwe rahisi kwa watendaji kutekeleza majukumu yao ipasavyo,kwa sasa serikali ya mtaa wa mivumoni kwa % mia wameshindwa kutatua changamoto za wananchi wa mivumoni kusini,mf miundo mbinu ya barabara na maji,wapiga kura wanataabika barabara hazipitiki na hawana maji kabisa,akina mama wanalazimika kufuata zaidi ya km kumi ili waweze kupata maji ya kisima ambayo kifya pia hayafai,ila hamna namna,

Address

Mivumoni Tegeta
Dar Es Salaam
255

Telephone

0786670232

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mivumoni kusini posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share


Other Performance & Event Venues in Dar es Salaam

Show All

You may also like