12/12/2017
UNAWEZA KUTOKA MAHALI ULIPO.
Kila jambo na wakati wake chini ya jua.
Kuna wakati wa kupanda na wakati wa kuvuna. Kuna wakati wa kulia na wakati wa kucheka.
Niliwahi kujiuliza k**a nyakati zisingebadilika ina maana masikini na wenye shida wangebaki na matatizo yao, na matajiri kadhalika.
Lkn mungu ni wa ajabu aliweka nyakati ili yule ambaye leo yuko juu akikosea kanuni za kuwa juu ashuke chini na yule anayetembea kwenye kanuni za mafanikio apande juu.
K**a unalia sana na umekata tamaa mwisho wa msiba wako umefika, umeteswa na umasikini na umejiapia utakufa nao maan huoni msaada. Wakati wa kulia., kuteswa na maumivu mengi unapita na unakuja wakati wako wa furaha wa kusahau taabu.
Cha kufanya ni kuzingatia kanuni muhimu zinazoweza kukutoa hapo ulipo na kukupeleka kwenye kicheko chako. Wale waliofanikiwa walizingatia kanuni za kuwa juu. Endelea kufuatilia page hii kila wakati utajifunza mengi zaidi
Barikiwa!!!
yako itatimia, thubutu #