Kilindo Boxing Club

Kilindo Boxing Club Mchezo wa ngumi (Boxing) ni aina ya michezo ya mapigano ambapo mabondia wawili wanapigana kwa kutumi

08/05/2023

in boxing you create a strategy to beat each new opponent, it's just like chess

14/07/2022

Ngumi Ulingoni, Punguzeni Mbwembwe..

23/06/2022
Kwa mujibu wa Taarifa kutoka Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Afrika ( WBF) limesema kuwa Bondia kutoka Tanzania Twaha Kid...
15/06/2022

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Afrika ( WBF) limesema kuwa Bondia kutoka Tanzania Twaha Kiduku ni Bondia namba nne kwa Ubora Afrika uzani wa Super Middleweight
1. RYNO LIEBENBERG (38) πŸ‡ΏπŸ‡¦
2. ISAAC CHILEMBA (35) πŸ‡²πŸ‡Ό
3. SENA AGBEKO (30) πŸ‡¬πŸ‡­
4. TWAHA KIDUKU (30) πŸ‡ΉπŸ‡Ώ
Ikumbukwe tu Twaha Kiduku mpaka sasa ana jumla ya mapambano 28 na ana nyota mbili huku akiwa anashika nafasi ya 96 kidunia kati ya mabondia 1,373

Bondia Hassan Mwakinyo ameporomoka kwa nafasi 16 kwenye viwango vya ngumi za kulipwa vya dunia sanjari na kupoteza nusu ...
09/06/2022

Bondia Hassan Mwakinyo ameporomoka kwa nafasi 16 kwenye viwango vya ngumi za kulipwa vya dunia sanjari na kupoteza nusu nyota.

Bondia huyo namba moja nchini ametajwa kuwa wa 33 duniani kwenye uzani wa super welter.

Awali Mwakinyo ambaye sasa anaishi Marekani alikuwa nafasi ya 17 mwenye nyota nne, akihitaji nyota moja kuingia kwenye orodha ya magwiji wa ndondi wa dunia wenye nyota tano wakitofautiana pointi.

Kwa mujibu wa mtandao wa ngumi za kulipwa wa duniani (Boxrec), Mwakinyo sasa ana nyota tatu na nusu.

09/06/2022

Baada ya video iliyosambaa ikimuonyesha bondia wa Afrika Kusini aliyefahamika kwa jina la Simiso Buthelezi, kumuacha mpinzani wake na kupigana na hewa, bondia huyo amefariki dunia kwa kilichothibitishwa kuwa ni kuvuja kwa damu kwenye ubongo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alipambana na mwenzake Siphesihle Mntungwa kuwania taji la WBF All Africa uzani mwepesi siku ya Jumapili mjini Durban, lakini pambano hilo la raundi 10 lilisitishwa na mwamuzi baada ya Buthelezi kuonekana kupigana na kivuli cha mpinzani asiyeonekana.

Picha za pambano hilo zilimuonyesha Mntungwa akianguka kupitia kamba na kisha, baada ya pambano hilo kuanza tena, Buthelezi alisonga mbele kuelekea kwenye kona tupu ambapo aliendelea kurusha ngumi.

Mntungwa alitangazwa mshindi na baadaye Buthelezi alianguka na kukimbizwa hospitalini. Aliwekwa katika hali ya kukosa fahamu baada ya kugundulika alikuwa anavuja damu kwenye ubongo.

Shirikisho la mchezo wa ndondi Afrika Kusini (BSA) lilithibitisha kuwa Buthelezi alifariki Jumanne jioni katika taarifa iliyotolewa kwa pamoja na familia ya bondia huyo.

07/06/2022

Piga Nikupige πŸ€œπŸ€›

07/06/2022

Maajabu katika Ring

06/06/2022

Funny Coacher 🏁
Usiige Mwanangu Utaumia kwa Makocha wa Kibongo..

06/06/2022

Sparring 🀼
Ngumi Moja Haina Ushindi, Combination Muhimu kwa Boxer katika Fight βœŠπŸ€›

08/10/2021
Tunakumbushana Kuwa Leo ndo Leo πŸ‘ŠMapambano ya Kibingwa Ndani ya Uwanja wa Tishio, Kilimahewa - Manzese Midizini Kuanzia ...
25/09/2021

Tunakumbushana Kuwa Leo ndo Leo πŸ‘Š
Mapambano ya Kibingwa Ndani ya Uwanja wa Tishio, Kilimahewa - Manzese Midizini Kuanzia Saa 11 Jioni.

Ndame Sports Promotion Wanakuletea Pambano la Ubingwa,Tarehe 25 September 2021, Siku ya Jumamosi.Litakalofanyika katika ...
14/09/2021

Ndame Sports Promotion Wanakuletea Pambano la Ubingwa,
Tarehe 25 September 2021, Siku ya Jumamosi.
Litakalofanyika katika Kiwanja cha Tishio - Manzese Midizini, Mtaa wa Kilimahewa.
Kuanzia Saa 11 Jioni,
Kiingilio Tsh 7000.

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kilindo Boxing Club posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Videos

Share


Other Sports Promoters in Dar es Salaam

Show All

You may also like